November 04, 2014

 
Stori: Makongoro Oging’
KIMENUKA! Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova, wiki iliyopita alifunguka kuwa, kuna watu wamekuwa wakimhusisha na imani ya Freemason.
Kamanda Kova aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa mkoa wake kuelekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.

 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani)
“Wananchi wanatakiwa kuwa makini na hawa watu ni hatari sana,wamekuwa wakitoa namba zao za simu na kuwatangazia wananchi wanaotaka kujiunga nao ili wawe matajiri wapige namba walizotoa ili wajiunge baada ya kutoa fedha, nashangaa hata mimi watu wameshawahi kuniita Freemason wakati siyo kweli,” alisema Kamanda Kova.
“Kwanza ninavyojua mimi Freemason anakuwa tajiri, anakuwa na mali nyingi sasa mimi nina mali gani mpaka watu waseme ni Freemason?” aling’aka Kamanda Kova. Kova hakufafanua ni kwa nini amekuwa akiitwa Freemason ingawa aliwataka wananchi wajihadhari na imani hiyo.
“Polisi wanatoa tahadhari kwa wananchi kwa watu wanaojiita Freemason na kutoa namba zao, hawa ni hatari sana, ni matapeli, hawafai ndani ya jamii, watashughulikiwa,” alisema Kova.Katika mkutano huo na waandishi wa habari Kova alisema kwamba msako mkali umeanza dhidi ya wahalifu na wale wote wanaovunja sheria ikiwa ni pamoja na madereva wa pikipiki na magari.


Chanzo:globalpublishers.info

Related Posts:

  • WATOTO 800 WALILAWITIWA 2013 Shirika hili linasema visa vya ukatili dgidi ya watoto TZ vimeongezeka Ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za binadamu nc… Read More
  • DIAMOND SASA COLLABO NA BEYONCE Hii Habari nimeisoma katika Gazeti moja Jana kuwa Diamond anahangaika kuwasiliana na Beyonce ili wafanye Wimbo Pamoja , Inasemekana Diamond alitafuta Number ya Beyonce kwa bahati nzuri akaipata na kumpigia simu na kum… Read More
  • WASANII TISA AMBAO HAWANA NIDHAMU BONGO 1. T.I.D Kauli mbaya na dharau ni kawaida kwake maneno kama mseeenge kuuuma na nk yanauhusiano mzuri na mdomo wake 2. Chidy Benz Ukisikia kampiga mtu alafu ukashangaa basi utakua mgeni nchini na labda kama hujawai … Read More
  • UTAFITI:WANANCHI WANAUNGA MKONO RASIMU YA KATIBA YA WARIOBA Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Twaweza umebainisha kuwa wananchi wanaunga mkono kwa kiwango kikubwa Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Wariob… Read More
  • SHAMBULIO LA BAMU LINGINE NAIROBI    Afisa wa polisi akilinda mojawapo ya maeneo katika jiji la Nairobi ambalo usalama wake unatatiza. Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari walilolizuia… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE