Leo Tarehe 2 dec 2014. kituo ch amatangao ya Radio cha Clouds Fm cha jijini Dar es Salaam kimeadhimisha miaka 15 tangu kuanza kurusha matangazo yake rasmi. Katika kumbukumbu hizo matukio mbalimbali yamefanyika leo hii ikiwa ni sehemu ya maazimisho ya miaka hiyo
Ambapo leo vipindi mbalimbali vya Clouds Fm vimekuwa na ugeni tofauti
tofauti ikiwemo Power Breakfast ambayo imemuhoji MD Joseph Kusaga
alieelezea changamoto mbalimbali walizokutana nazo kwenye hii miaka 15
ya Clouds FM na mafanikio pia.
Wengine ni waliokuwa watangazaji wa Power Breakfast Masoud Kipanya na
Fina Mango ambapo leo walikua live kwenye Power Breakfast, ambapo
kwenye Leo Tena kuna ugeni wa Khadija Kopa, Diamond Sound na Tx Junior.
WADAU WANENA:
Malkia wa Mipasho Tanzania,Hadija Kopa akiwa kwenye kipindi cha Leo Tena naye akizungumzia miaka 15 ya Clouds FM
Mama Siza wa Segere akiwa kwenye kipindi cha Leo Tena naye ni mmoja wa wasanii wa zamani waliotolewa na Clouds FM akizungumzia miaka 15 ya redio ya watu.
Waanzilishi wa bendi ya Diamond Music,Alan Mulumba na King Dodoo wakiwa mjendoni clouds fm wakizungumzia sherehe za miaka 15 ya Clouds.
Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena,Dina Marious akizungumzia miaka 15 ya Clouds FM.
Zamaradi Mketema.
Watangazaji
wa zamani wa Clouds FM,Masoud Kipanya na Fina Mango wakizungumzia miaka
15 ya redio ya watu kwenye kipindi cha Power Breakfast wakiwa na
mtangazaji wa kipindi hicho,Gerald Hando
Waziri Njenje aka Babu Njenje naye alikuwepo mjengoni kwenye sherehe za miaka 15 ya Clouds fm.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumzia miaka 15 ya Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast leo na Gerald Hando,ambapo kauli mbiu ya sherehe ya mwaka huu ni #TunakufunguliaDunia #KuwaUnachotaka
0 MAONI YAKO:
Post a Comment