December 30, 2014

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Valentino Mlowola
Nchini Tanzania katika Kijiji cha Ndami, tarafa ya Mwamashimba wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza watu wasiofahamika wamevunja nyumba na kumteka mtoto mwenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino na kutoweka naye.
Watu hao walivamia nyumba ya wazazi wa mtoto Pendo Emmanuel, mwenye ulemavu wa ngozi wakiwa na mapanga na kisha kutoweka naye gizani baada ya kuwazidi nguvu wazazi wake.
Emmanuel Shilinde mzazi wa mtoto huyo ameieleza polisi kuwa majira ya saa nne usiku watu wawili waliuvunja mlango wa nyumba yake kwa jiwe wakamchukua mtoto kwa nguvu kisha wakakimbilia gizani kwa pikipiki.
Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi mkoani mwanza Valentino Mlowola , ameitaarifu BBC kuwa leo ni siku ya tatu na polisi bado ina matumaini ya kumpata akiwa hai motto huyo, kwa kuwa bado hawajaupata mwili wake akiwa amepoteza uhai. Msako unaendelea na tayari kuna watu watano wanazuiliwa na polisi ili kusaidia kufahamu mtoto huyo yuko wapi.
Takwimu za kuanzia mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wamepata ulemavu mwingine wa kudumu.

Related Posts:

  • MWANAFUNZI AKUTWA AKIFANYA NGONO NA NGÓMBE WA JIRANI!!  Binafsi imenisikitisha sana.... na nimestaajabika mno. Habari na Ezekiel Kamanga, KyelaMwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Ikolo, Wilaya ya Kyela Bakiro Hance (18), amekutwa akifa… Read More
  • TB JOSHUA: UTABIRI WAKE WATIMIA Prophet TB Joshua alitabiri mwaka jana kwamba Nigeria itakua ya kwanza kiuchumi kushinda nchi zote za Africa. Wakati anatabiri. ..nilikua nikiangalia nchi ya Africa Kusini, Misri etc.....niliwaza sana. Jana Imetangazwa kuw… Read More
  • MVUA ZALITESA JIJI LA DAR Mburahati na Mayfair leo asubuhi Tokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam, zimepelekea uharibufu wa barabara na mazingira. Haya ni maeneo ya jiji la Dar es Salaam yaliyoathirika … Read More
  • MTAZAME JUX AKIFANYA VIDEO YA NITASUBIRI NCHINI CHINA   Msanii Jux wa bongofleva kabla hajaondoka kwenda China safari hii, alisema atautumia muda wake akiwa huko kushoot video ya wimbo wake mpya “nitasubiri” ambao wiki kadhaa zilizopita alikiri kwamba wimbo huo … Read More
  • PATA MUDA WA KUANGALIA VIDEO MPYA YA QUEEN DARLEEN NA SHILOLE   Hii ni video iliyowahusisha Diamond Platnumz na dada yake wa damu  Queen Darlin uzinduzi wa video hii ulifanyika Bilicanas mwishoni mwa wiki iliyopita,video hii imetenegezwa na kampuni ya Jerry Mushala Stud… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE