December 18, 2014


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka amegoma kujiuzulu kwakuwa haoni sababu ya kufanya hivyo
Akiendelea kuzungumza na waandishi muda huu anasema watu wanaona kujiuzulu ni 'fashion' ila yeye hayuko katika 'fashion' hiyo

“Mimi Nijiuzulu kwa sababu gani? yaani kwa sababu ya mafanikio ya kuwakomboa wanawake kwenye Elimu ndio mimi nijuzulu,maana kujiuzulu kunasababu, na hakuna sababu ya mimi kufanya hivyo na sitofanya hivyo kwani wanaodai mimi nijiuzulu ni wanafiki wenye nia mbaya na mimi ,na mimi sijiuzulu ng’o na nikifanya wanavyotaka Rais atashangaa ”alisema Waziri Tibaijuka.
“Leo natuhumiwa na kila mtu kwamba nimepewa pesa na Rugimalira kwamba ni za kifisadi,Jamani tuwe wa kweli kuhusu madai haya maana nimepewa pesa na Rugemalira kwa ajiri ya shule hizi na sio huyo pekee alliyechangia kwani waliochangia pesa hizi ni watu wengi ikiwema Rais wa Awamu ya Tatu,Benjamin Mkapa,Mfanya Biashara Maarufu Reginald Mengi na wengine wengi,inakuwaje leo mchango wa Rugumarila kwa Ajiri ya Elimu kwenye Shule hii ndio iwe nongwa”
“Kwasababu ukisema ni pesa alizonipa ni za ufisadi wa Escrow sio kweli,kwani Bodi ya Shule ilimuomba Bwana Rugemalira pesa kwa kutumia Kampuni yake ya Mabibo Wine na kipindi kile ndio alikuwa kiongozi, sasa hawa watu wanaozani ni za ufisadi inakuwaje jamani tuwe wakweli”Aliongeza Waziri Tibaijuka."

Related Posts:

  • CAF: Club kujigharamia Malazi   Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefanyia marekebisho kanuni zake za michuano ya ngazi ya klabu kwa upande wa malazi ambapo sasa timu zitachagua na kujilipia zenyewe hoteli zinapokuwa kwenye mechi za u… Read More
  • Bangi halali kwa matibabu Jamaica    Baraza la mawaziri la Jamaica, limeidhinisha mswada ambao unahalalisha watu kumiliki kiwango kidogo cha Marijuana. Ina maana kwamba hii ni mara ya kwanza kwa jamii ya 'Warastafarian' wanaotumia Bangi kwa sa… Read More
  • WhatsApp yawabana watumiaji Mtandao wa WjhatsApp Mtandao wa kijamii wa What… Read More
  • Official HD Music Video-Y-Tony ft Barnaba - Mama Msanii wa bongo fleva anaekuja kwa kasi katika soko la muziki wa bongo,mwenye hit song ya masebene,ameachia video yake mpya aliyo mshirikisha Barnaba nyimbo inaitwa Mama Utengenezwaji wa video hii ulianza mwaka jana… Read More
  • Tunda man "Rais wa Tanzania ni Lowassa tu"    Mwana muziki toka katika kundi la Tip Top Connection la Manzese Tunda man, anasema kwa sasa Tanzania inahitaji kiongozi anayeweza kuendana na wakati wa sasa.   Akizungumza na Ubalozini.blogspot.co… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE