December 30, 2014

Gone to the Pub

Hekaheka iliyosikika kwenye show ya Leo Tena ya Clouds FM, imetokea Mbezi, Dar es Salaam.

Wanawake wawili wamelalamikia kitendo cha dada mmoja ambaye amefungua pub ya kuuza vinywaji, lakini wanawake hao wamesema kuwa mwanamke huyo ameweka magodoro mawili ambapo ametuhumiwa kuwa anawalaza wanaume za watu ndani ya Pub hiyo.

Mwanamke mmoja amesema kuwa waliuza nyumba na mumewe na wakaamua kujenga nyumba nyingine lakini mwanaume huyo alimtelekeza mkewe eneo la ujenzi na kwenda kunywa pombe katika Pub hiyo, alipomfuata mwanaume huo aligoma kuondoka hivyo mwanamke akaamua kumwaga vinywaji vilivyokuwa kwenye meza na kupelekea ugomvi kati yao.

Wanawake hao waliandamana kwenda kwenye Pub ya mwanamke huyo ili wakamseme kuhusu tabia hiyo, lakini mwanamke huyo alikataa kuwa huwa anawalaza wanaume hao katika Pub yake, ila magodoro ambayo yapo huwa wanayatumia wafanyakazi wake kulala wakati wa usiku.

Unaweza kuisikiliza Hekaheka hiyo kwa kubonyeza play hapa.

Related Posts:

  • LIVE: Barcelona VS Juventus   Muda huu kuna mpambano unaoendelea kati ya Barcelona na Juventus. Tumekuwekea hapa waweza kufwatilia mpaka mwisho ili uweze kujua nini kinajiri katika mpambano huu        &nbs… Read More
  • New Video: P-Square - Nobody   Kutoka nchini Nigeria P-Square wametuletea video mpya kabisa inaitwa, Nobody. Video ipo hapa chini waweza kuitazama na kudownload sasa kupitia Youtube.          &nbs… Read More
  • Tweet ya Prof. J kuhusu Millard Ayo hii hapa   Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya CHADEMA Joseph Haule Prof, J, amempongeza mtangazaji wa Clouds Media Millard Ayo kwa kutoa habari zake na kupaza sauti za wanyonge.  Prof J ametweet leo hii  Joseph L.… Read More
  • Point za mezani na Mitazamo ya Rage Ismail Aden Rage-Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba SC Mwenyekiti wa zamani wa Simba Alhaj Aden Rage ameungana na wadau wengine kupinga matokeo ya mezani kwakua kuna njia nyingi za kuweza kuepuka timu kupewa au kupokw… Read More
  • Mwizi wa simu anaswa kwa kutumia App   Mshukiwa wa wizi ambaye inaaminika alikuwa ameiba zaidi ya simu 100 aina ya iPhones amekamatwa nchini Marekani. Mwizi huyo alikamatwa baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kutumia programu tumishi ya Find My … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE