January 14, 2015

Ziwa Tanganyika.
Ziwa Tanganyika.
Abiria 60 kutoka Burundi na Jamhuri  ya Kidemokrasi  Ya Congo – DRC walionusurika katika ajali ya kuzama kwa boti katika ziwa Tanganyika wamewashukuru watanzania kwa kuwaokoa na kuwapatia misaada ya kibinadamu.
Wakizungumza  kutoka  kijijini  Sigunga wilayani Uvinza mkoani Kigoma wamesema ukarimu ulioonyeshwa na watanzania kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa unapaswa kuigwa na nchi zao.

Maafisa kutoka idara ya uhamiaji mkoani Kigoma walikuwa ni miongoni mwa wataalam waliokuwemo kwenye msafara ulioongozwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Kigoma Ramadhan Maneno ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kigoma ambapo baada ya kuwasili Sigunga walifanya sensa ya kuandisha majina na uraia wa abiria walionusurika.
Sensa ikabaini abiria 81 ambapo 34 kati ya hao ni kutoka Burundi, 17 kutoka DCR na 34 ni Watanzania ambapo 31 kati ya hao wanatokea mkoani Rukwa.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE