January 05, 2015




Papaso Ni kipindi Kipya Cha Radio TBC fm Kilichoanza Mwaka huu 2015 Toka Tarehe 1 January.

Lengo La Kipindi ni Kuburudisha,Kutoa Elimu nk.


Hapa Chini Nimekuwekea Mpangilio Mzima Wa Kipindi.
Ama Kwa Uhakika Hutojutia Kusikiliza Kipindi Hiki Kutoka Kwa BabaMzazi Djaro Arungu.


JINA LA KIPINDI: PAPASO !

HOST: D’JARO ARUNGU

KAULIMBIU: TUNAPAPASA KILA KONA.

STATION:TBC FM

MUDA;SAA 1JIONI-4USIKU.


MAANA YA KIPINDI!
PAPASO inatokana na kitendo cha KUPAPASA…. Unapopapasa hujui ni kipi utashika na kipi hautashika. Hivyo katika papaso tunapapasa kila kona ili kukidhi kiu ya msikilizaji. Muziki utapapaswa, wanamuziki, wasanii wa maigizo, mitaa itapapaswa, simulizi zitawapapasa wasikilizaji.Maswali nk

Majibu baada ya papaso ni burudani, faraja Na Kutoa elimu Kwa Jamii.

YALIYOMO KATIKA PAPASO !

1. TANO ZA PAPASO 
(Dak. 30 saa 1 hadi saa 1 na 30

*Nyimbo 5 chaguo la ‘host’ zitachezwa.

2.PAPASO ZA LEOLEO 
(Dakik. 15 saa 1;30 hadi saa 1:45)

*Nyimbo mpya mbili/tatu MPYA au zilizotoka ndani ya siku chache zilizopita zitachezwa na host wa kipindi.

MFANO:

Mwana Dar-es-salaam- Ally Kiba

N’tampata Wapi- Diamond Platinumz.

3. (Dakika 15. Saa 1:45 hadi saa 2:00)

i. IPO HIVI: Kipengele ambacho kinazungumzia ‘FACT’mbalimbali za kidunia ambazo watu wengi hawajawahi kukutana nazo.

Mfano:

**IPO HIVI- Mwanadamu wa kawaida husema UONGO walau mara nne kwa siku mara 1460’kwa mwaka na mara 88,000 ndani ya miaka sita. Na uongo mkubwa ni huu.

Una matatizo kisha mtu anakuuliza. Habari za asubuhi unajibu ‘NJEMA tena Ukitabasamu.

**IPO HIVI- KILA baada ya miaka saba, unapoteza nusu ya marafiki wako wa muda mrefu na nafasi hizo kuchukuliwa na marafiki wapya. Rafiki anayedumu baada ya miaka saba huitwa RAFIKI MADHUBUTI.

**IPO HIVI- Kisaikolojia kumwona rafiki yako amebadilika haiumizi sana kinachoumiza ni zile kumbukumbu za alivyokuwa awali kabla hajabadilika.


ii. CHIMBO LA PAPASO.

Chimbo inatoka Kwenye Neno Chimba.Hapa Tutachimba Vitu ambavyo Zimejificha Chini Na Kuziibua.Vitu Ambavyo Watu Hawajui.

Katika kipengele hiki italetwa makala fupi sana, makala yenye kitu cha kipekee sana ambacho kitawaacha wasikilizaji midomo wazi.

Mfano!

HACHIKO- Mbwa mwenye pendo la dhati na mtiifu kupita wote duniani.

Alizaliwa mnamo mwaka 1923 nchini Japan na kufariki mwaka 1935. Anakumbukwa kwa pendo lake la dhati kwa mmiliki wake bwana Hidesaburo Uweno.

Hachiko alipewa malezi mazuri na mmiliki wake ambaye alikuwa mkufunzi wa chuo kikuu nchini Japani.

Mkufunzi huyo alimzoesha Hachiko kuwa anamsindikiza hadi kituo cha Treni ambapo alipanda treni kuelekea kazini. Na alipokelewa na Hachiko kila alipokuwa akitelemka wakati wa kurudi.

Siku moja mkufunzi aliondoka akisindikizwa na Hachiko. Lakini ule muda wa kurejea hakushuka katika Treni.

Mkufunzi alikufa akiwa anafundisha!!

Tangu siku hiyo na hadi kifo chake Hachiko aliendelea kwenda kituo cha Treni kumsubiri mmiliki wake akiamini ipo siku atarejea.

Hachiko hakufanya jambo jingine katika maisha yake hadi alipopoteza uhai wake….

Nchini Japani amejengewa sanamu!!

Naam! Mbwa muaminifu, mtiifu na mwenye upendo kupita wote duniani.

HACHIKO.




SAA MBILI KAMILI ( MUHTASARI WA HABARI)

4.KUZUNGUMZA NA WADAU/ SOCIAL NETWORKS.

(Dak. 8 saa 2:02 hadi 2:10)

Hapa watapiga simu, watatuma jumbe fupi. Na muda huu habari mbalimbali kutoka mitandaoni zitasomwa!!!

5. PAPASO MTAANI. (Dak. 15, saa 2:10 hadi 2:25)

Kila kona ya mtaani itaguswa hapa.

-Mahojiano na wasanii wa muziki mtaani.

-Story zinazobamba mtaani

-Story za muziki na UCHAMBUZI.


6.SIMULIZI ZA PAPASO.

(Dakika 5:00 Usiku Saa 2:25 hadi saa 2:30Usiku)

-Hapa zitakuwepo simulizi Fupi na kali. Zinazogusa hisia na kuelimisha kwa kiasi kikubwa sana.

7. RADIO JAPAN. 
(Dakika 30. Saa 2:30Usiku hadi Saa 3:00Usiku)

Hapa TBC FM itajiunga moja kwa moja na Matangazo Kutoka Radio Japan.


8. PAPASO PASUA KICHWA !

(Dakika 40. Saa 3:00Usiku hadi Saa 3:40Usiku)

Maana ya Pasua Kichwa ni Kufikiria Kwa Makini !

Huu ni Muda wa Maswali na Majibu (Chemsha Bongo) Mtangazaji anatoa swali kwa Msikilizaji na akipata anapata nafasi ya Kutuma Salamu Kwa Watu Watatu.Inabidi atumie akili na Kufikiria kwani unaweza dhani Swali ni Rahisi kumbe la Mtego Ndio Maana Tukaita PAPASO PASUA KICHWA.

Papaso Pasua Kichwa itaambatana Pia na Burudani Safi Ya Muziki.
9.PAPASO KIZUNGUMKUTI !

(Dakika 10. Saa 3:40Usiku Hadi Saa 3:50Usiku)

Maana Ya Kizungumkuti ni Dilema,Sintofahamu,Kitu au Jambo linalochanganya.

Hapa nitawaletea Swali 1 Kwa Siku linalochanganya Kidogo na Watumie Muda wa Kufikiria na Kutoa JIBU au Suluhisho.

Mfano! Bwana John Ameenda Ukweni Na Mke Wake Na mfukoni ana shilingi elf 50 Ambazo Sio zake ni za Bwana Juma ambaye ni Mkorofi Ajabu na Hizo hela inatakiwa Akitoka tu Ukweni amperekee Bwana Juma.Kama Sio Mke Wake Kumlazimisha Basi angemperekea Kwanza Bwana JUMA hela Zake.

Kufika Ukweni hali Tete Mbaya sana.Anaombwa na MAMA Mkwe shilingi elf 10 tu.John anakataa kata kata kuwa hana hata senti 5 Kwa Sababu anajua Ukorofi wa Juma.MAMA Mkwe Kwa Shingo Upande anakubaliana Na John.

Kutoka tu Baada ya Kuaga anagundua amedondosha sh elf 10 Pale kwenye Kochi.

Je,Kama wewe ndio Bwana John Utarudi Kuichukua Hiyo Hela au?

Kumbuka alimwambia MAMA MKwe hana hata senti 5 na Mke wake Pia anajua Hivyo.

Tumsaidie Bwana John.

10. PAPASO CHAPCHAP ! (Dakika 10. Saa 3:50Usiku hadi saa 4:00usiku.)

Hapa ni Kuvunjika Mbavu na Zile Salaam za Haraka Haraka(Salaam za ChapChap)Wengi hawana spidi ya kusema maneno Haraka Haraka,inatakiwa Chini ya Dakika 1 usalimie hata Watu 20.Hapa Tukisema Spidi Ni Spidi Kweli Kweli kWA Msikilizaji Ni Bonge 1 la Burudani.

PAPASO SPECIAL.
JUMANNE: Patakuwa na mahojiano na msanii wa Aina Yeyote Yule au Mdau wa Kawaida atakuja studio na kuhojiwa live Kutokana na Kinachomhusu Pamoja na Mambo Mengine Mengi za Kijamii nk.

IJUMAA: Patakuwa na KUMI BORA ZA PAPASO. Kuanzia saa moja kamili hadi saa mbili usiku.

Nyimbo ambayo inachaguliwa sana na wasikilizaji itapanda ama kushuka ikiwa haichaguliwi sana.

MOST WANTED: Msanii aliyepotea kwenye game muda mrefu akipatikana kona yoyote ile ya papaso lazima apapaswe na kusalimiana na wasikilizaji wake.

Au hata Mtu au Mdau yeyote Ambaye Tunaona anatufaa Kufanya naye Mahojiano ili Tujuwe Kitu.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE