KIKUNDI
kinachodaiwa kuwa Panya Road kimetikisa maeneo mbalimbali ya Jiji la
Dar es Salaam kwa kupora mali, kujeruhi watu na kuzua sintofahamu katika
maeneo ya jiji hilo wakiwa na mapanga mikononi.
Maeneo
yaliyokumbwa na dhooruba hiyo ni pamoja na Sinza, Tandale, Mwananyamala
na maeneo mengineyo usiku huu. Maduka na baa zimefungwa na kupelekea
polisi kupiga risasi hewani kuwatawanya watu waliokuwa wamekaa
kimakundimakundi.
Imeelezwa
kuwa fujo zilianzia mchana wa jana baada ya kiongozi wa Panya Road aitwaye
Diamond kuuawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani
usiku wa kuamkia mwaka mpya kwa kukatwakatwa na mapanga.
Baada ya kumzika mwenzaoleo, vijana hao wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo.
Usiku ulipoingia wakaanza kazi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Jiji la Dar.
Baadhi
ya mashuhuda walioshuhudia matukio hayo wanadai vijana hao walikuwa na
silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na walivamia maeneo kadhaa zikiwemo
baa.
Wateja
waliokuwa katika baa ya Calabash iliyopo maeneo ya Mpakani, Mwenge
walilazimika kuacha vinywaji vyao na kukimbia hovyo huku wengine
wakikanyagana na kukatwa na vipande vya chupa kwa kile kilichodaiwa kuwa
vijana hao walikuwa wanakatiza maeneo hayo japo hawakuingia ndani.
Baada
ya tukio hilo wateja wengi waliamua kurudi majumbani kutokana na baadhi
yao kujeruhiwa na vipande vya chupa wakati wakikimbia
0 MAONI YAKO:
Post a Comment