Makamanda
wa polisi wa mikoa mitatu ya simiyu, shinyanga na mwanza wamefanikiwa
kuvunja mtandao hatari wa ujambazi uliokuwa unaongozwa na mfanyabiashara
wa mjini bariadi Njile Samwel huku makachero wa jeshi hilo katika mikoa
ya kanda ya ziwa pia wakikamata watuhumiwa watano, bunduki moja ya SMG,
risasi 331 na mifupa inayodaiwa kuwa ya binadamu.
Kamanda
wa polisi mkoani mwanza, SACP Valentino Mlowola, akiwa ameambatana na
kamanda Justus Kamugisha wa mkoa wa shinyanga pamoja na Charles Mkumbo
wa mkoa wa simiyu wanajitokeza kwa waandishi wa habari kuelezea tukio la
kukamatwa kwa njile samwel ambaye amekuwa na tabia ya kunzisha mtandao
wa uhalifu na kisha kuwaua kama mbinu ya kukwepa wapelelezi.
Kuhusu tukio la kutekwa kwa mtoto pendo emanuel mwenye ulemavu wa ngozi wa ngozi lililotokea desemba 27 mwaka jana katika kijiji cha ndami wilayani kwimba., kamanda wa polisi mkoani mwanza valentino mlowola amesema polisi inaendelea kuwashikilia watuhumiwa wanane akiwemo baba mzazi wa mtoto huyo baada ya mchujo kufanyika huku akisema jeshi hilo halitashindwa kumpata mtoto huyo akiwa hai au hata amekufa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment