January 05, 2015


Marianna_Graves0 
Hekaheka ya leo January 5 inatoka Shinyanga ambapo ndugu wa mwanamke mmoja aliyefariki walimpasua tumbo marehemu huyo na kumuwekea kifaranga cha kuku kikiwa kizima.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa marehemu alifariki akiwa na tatizo la uvimbe tumboni, makubaliano yao ilikuwa kwamba wafanye shughuli hiyo wakati mwili wa marehemu akiwa hospitali lakini mtafaruku ukazuka pale ambapo ndugu hao waliamua kufanya zoezi hilo wakati jeneza limeshushwa ndani ya kaburi.

Watu waliamua kususia mazishi baada ya mtu huyo ambapo ndugu wakaamua kufanya mazishi hayo wenyewe ambapo Polisi waliingilia kati pia kujua chanzo cha mtafaruku huo.
Mzshi
Imesemekana mzozo wa mazishi hayo ulitokana na kijana aliyemuoa mwanamke huyo kutotoa mahari hivyo ndugu hao wakataka wapewe pesa kiasi cha mil.2 ili waruhusu mazishi hayo yafanyike.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE