January 15, 2015

Kansela Angela Merkel

Kansela Angela Merkel
  Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ameahidi kuwalinda Wayahudi na Waislamu wanaoishi nchini Ujerumani dhidi ya ubaguzi.
Amesema demokrasia ndiyo njia bora ya kupambana na machafuko yanayofanywa na watu wenye misimamo mikali, kama yale matukio ya nchini Ufaransa wiki iliyopita.
Kauli hiyo ameitoa leo baada ya bunge la Ujerumani-Bundestag, kuwakumbuka kwa dakika moja wahanga 17 waliouawa katika mashambulizi ya wiki iliyopita mjini Paris. Merkel amesema Uyahudi na Uislamu vyote ni sehemu ya Ujerumani na ameahidi kwamba suala la kupambana na Uyahudi na mashambulizi dhidi ya misikiti litakuwa na mashtaka sawa.
Akizungumza wakati wa kikao hicho cha bunge kilichohudhuriwa na balozi wa Ufaransa nchini Ujerumani na viongozi wa kidini, Merkel amesema Ujerumani na Ufaransa zinahusiana kutokana na urafiki muhimu walionao.
''Ujerumani na Ufaransa zinasimama pamoja wakati wa matatizo haya magumu. Ujerumani na Ufaransa zinasimama pamoja zikijua wazi kwamba Ujerumani haiwezi kuwa na usalama, iwapo hakuna usalama Ufaransa, alisema Merkel .''
Kansela Merkel amesema ni muhimu pia kwa viongozi wa dini ya Kiislamu kuandaa mwongozo wa wazi unaotofautisha kati ya Uislamu na ugaidi. Amesema watu wengi nchini Ujerumani siyo maadui wa Uislamu, ingawa watu wanataka kujua ni kwa nini magaidi hawana huruma na maisha ya binaadamu.
Merkel na wabunge wa Ujerumani wakiwakumbuka wahanga wa Paris Merkel na wabunge wa Ujerumani wakiwakumbuka wahanga wa Paris
Amesema viongozi hao wanapaswa kueleza ni kwa nini mara nyingi ghasia zinafanyika kwa kutumia imani yao.
Ujerumani haitoyumbishwa na vitendo vya itikadi kali
Amebainisha kuwa Ujerumani haitoyumbishwa kwa vitendo vya itikadi kali na itahakikisha inapambana na mahubiri ya chuki, vurugu na ghasia zinazofanywa kwa kutumia jina la Usialmu na wale walio nyuma ya ghasia hizo. Merkel amesema hatua zilizochukuliwa na Ujerumani na Ulaya ili kuweka ulinzi dhidi ya kitisho cha ugaidi na Uislamu wenye itikadi kali, hazitowaruhusu magaidi kuigawa jamii.
Amesema baada ya kufanikisha hatua ya kupiga marufuku watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Jihadi, baraza lake la mawaziri litaweka adhabu kali kwa watu wanaofadhili ugaidi. Hata hivyo, Ujerumani itaendelea kutoa msaada wa silaha na mafunzo ya kijeshi kwa majeshi ya Wakurdi wanaopigana na kundi lenye itikadi kali linalojiita Dola la Kiislamu-IS, nchini Iraq na Syria.
Aidha, Kansela Merkel ameunga mkono wazo la kuwepo uchunguzi zaidi wa data za mtandaoni ili kupambana na ugaidi na katika hatua za kuhakikisha usalama. Ametoa wito wa kuanzishwa upya hatua za kuwaruhusu maafisa kuficha data, suala ambalo wakosoaji wanasema huenda likahujumu uhuru wa vyombo vya habari na kukiuka haki za kimsingi za umma.
Mashambulizi ya Paris yametokea wakati ambapo Ujerumani ikitathmini namna ya kukabiliana na maandamano katika mji wa mashariki wa Dresden yanayoongozwa na kundi linalopinga Uislamu linalojiita PEGIDA.

Related Posts:

  • ONA HUYU DADA ALIVYOADHIRIKA KUTOKANA NA DHALAU Leo Asubuhi Nikiwa Ubungo bus terminal.... Leo asubuhi nikiwa stand ya mabasi ya ubungo,mdada mmoja wakati anapanda kwenye kagari kake akadondosha simu.Mimi nikamuita ili nimweleze kilichotokea,akanisonya tena msonyo wa… Read More
  • UNYAMA HUU NI NOMA KWA KWELI Na Haruni Sanchawa MKE wa rais, mama Salma Kikwete alizungumza kweli kwamba, mtoto wa mwenzio ni wako! Lakini sivyo kwa mtoto Suleiman Riziki (4), mkazi wa Pugu Kinyamwezi, jijini Dar es Salaam ambaye amejikuta katika w… Read More
  • KAMA UNATUMIA WHATSAPP BASI HII INAKUHUSU Whatsapp ni moja kati ya makampuni makubwa sana duniani hivi sasa,inadhaniwa kuwa na watumiaji wengi sana duniani hivi sasa kuizidi hata facebook,jambo lililofanya mmiliki wa facebook kuona umuhimu wa kuinunua kwa… Read More
  • DUH!!!! HII INATISHA SASA, KUKUTA JENEZA NJE KWAKO!!!   Mke anasema hii sio mara ya kwanza kwa wao kukuta jeneza dogo likiwa na paka ndani yake ambapo wakati uliopita alichukua hilo jeneza na kwenda kuchoma kisha baada ya siku mbili akakutana na kitu kilekile ml… Read More
  • SHILOLE KUFANYA BIASHARA   Hit maker wa Nakomaa na Jiji Shilole ame-amplify taarifa za kuhusu kufungua mgahawa wake ambao ameupa jina la wimbo wake mpya uitwao  Chuna buzi cafe anatarajia kufungua mgahawa wake wa chakula maeneo ya nyu… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE