
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2,
2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es
Salaam.
Kabla ya uteuzi wake,
Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju
pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania
0 MAONI YAKO:
Post a Comment