February 25, 2015

Wanajeshi wa jeshi la Chad katika mitaa ya mji wa Gamburu, Nigeria, Februari 4 mwaka 2015. 

Jeshi la Chad limebaini kwamba ngome zake zimeshambuliwa na wapiganaji wa Boko Haram Jumanne Februari 24, karibu na mji wa Gambaru, nchini Nigeria. Jeshi la Chad limejibu shambulio hilo, na hasara iliyotokea ni kubwa kwa upande wa Boko Haram.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi tulivyowasiliana kwenye uwanja wa mapigano, wapiganaji wa Boko Haram ndio walioanza kushambulia ngome za jeshi la Chad. Wakati huo huo jeshi la Chad lilijibu shambulio hilo, na kuwatimua wapiganaji hao hadi katika kijiji kilio karibu na msitu unaopakana na mji wa Gambaru.
Mapigano, makali kwa mujibu wa vyanzo vya RFI, yanasadikiwa kuwa yalidumu masaa kadhaa. Uchunguzi wa kwanza unaonesha kuwa wapiganaji 207 wa Boko Haram wameuawa, huku jeshi la Chad likimpoteza mwanajeshi wake mmoja na wengine tisa wamejeruhiwa.
Jeshi la Chad limethibitisha kwamba limeteketeza magari na pikipiki zaidi ya 20 ambayo yalitumia na Boko Haram kwa kuendesha shambulio hilo. Kwa mujibu wa jeshi la Chad, silaha nzito za kivita na vifaa vingine vya kijeshi zimekamatwa.
Mfululizo wa mashambulizi Kano
Hayo yakijiri, watu 27 wameuawa Jumanne wiki hii katika mfululizo wa mashambulizi yaliyolenga kituo cha mabasi kaskazini mashariki mwa Nigeria, ikiwa imesalia majuma matano kabla ya uchaguzi mkuu Machi 28.
Mashambulizi hayo yaliendeshwa Jumanne mchana wiki hii katika mji wa Kano na watu wawili ambao walikua wakishuka basi.
Saa chache kabla, katika mji wa Potiskum, mji mkuu wa kiuchumi wa jimbo la Yobe, kulitokea shambulio ambalo lililenga basi lililokuwemo abiria wengi katika kituo cha mabasi nje kidogo ya mji.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE