Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limewakamata wahamiaji haramu 13
kutoka nchini Ethiopia wakiwa kwenye gari ndogo aina Prado katika
kijiji cha Lusanga Turiani wilayani Mvomero wakijiandaa kwenda Afrika
kusini kupitia mkoani Mbeya .
Kamanda
wa polisi mkoa wa Morogoro ACP leonard Paul
akizungumzia tukio hilo
amesema waethiopia hao walitokea nchini Kenya na kupita Handeni na
kuingia wilayani Mvomero na walikuwa wakijiendaa kwenda Mbeya kabla ya
kwenda nchini Afrika Kusini kutafuta hifadhi.
Jeshi hilo pia linamshikilia dereva wa gari hiyo na wanafanya
mawasilinao na idara ya uhamiaji na baada ya upelelezi kukamilika
watafikishwa mahakamani.
Naye dereva wa gari ndogo aina ya Prado Musa Edmund akiongea huku
akionekana kuficha sura yake anayeshikiliwa kwa kusafirisha waethiopia
hao amesema alimpeleka boss wake Arusha njiani wakati anarudi alikutana
na waethiopia hao mbapo waliomba awasafirishe kwa makubalinao kuwa
atalipwa shilingi milioni moja hadi kuwafikisha mkoani Mbeya ambapo
alilipwa nusu ya gharama hizo kwa makubalino malipo mengine yangefanyika
baada kuwafikisha mkoani Mbeya
0 MAONI YAKO:
Post a Comment