February 26, 2015

 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia huru mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya shilingi laki tisa sh:900,000/=.
 Awali Chidi Benzi alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela ama kulipa faini ya kiasi hicho cha pesa kufuatia kesi iliyokuwa ikimkabili ya  kukamatwa na madawa ya kulevya.
 Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya,aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh: 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae. Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE