Bwana huyo ambaye
taswira yake akiwachinja mateka kwa kisu bila huruma ndiyo nembo ya
wapiganaji hao sasa ametambuliwa kuwa anatokea Uingereza.
Shirika la Habari la BBC limetambua kuwa jina lake kamili ni Mohammed Emwazi.
Emnuazi
ameonekana kwenye video kadhaa ya mauwaji ya mateka wa mataifa wa
magharibi, akiwemo Mmarekani James Foley, Raia wa Uingereza, Alan
Henning na mwaandishi habari wa Japan, Kenji Goto.
Inaaminika kuwa Emwazi ni raia wa Uingereza na hasa anatokea magharibi mwa London.
Yamkini
Emnuazi aliyezaliwa Kuwaiti na mwenye umri wa kati ya miaka 20 -29
alikuwa amefahamika sana na vyombo vya usalama lakini kwa sababu za
kiusalama haikuwezekana kumtambua.
Anaaminika amewahi kuishi Somalia mnamo mwaka 2006 na anauhusiano mkubwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabab nchini humo.
Polisi
nchini Uingereza imeziomba vyombo vya habari kutosambaza habari ambazo
hawajazithibitisha kumhusu jamaa huyo kwani uchunguzi unaendelea.
Hata hivyo bado habari za kina kumhusu Jihadi John hazijatolewa.
Mwandishi
wa maswala ya Usalama wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa vyombo vya
usalama vya serikali za mataifa yanayokaribia Somalia sasa yana kila
sababu ya kutahamaki.
Kwa sababu Kuhusika kwake na kundi la Al Shaabab kisha akajiunga na kundi la Islamic State ambalo kwa wakati mmoja lilikuwa linashindana na wanamgambo wa Al Qaeda kuhusu yupi kati yao anayeushawishi
mkubwa
Ishara kuwa Al Shabab inazingatia msimamo mkali wa kidni hata zaidi ya Al Qaeda.
Kwa sababu itakumbukwa kuwa Al Qaeda ilipinga hatua kali ya kuwachinja mateka nchini Iraq na Syria.
Emnuazi ambaye amekuwa akiwabeza mataifa ya Magharibi kabla ya kuwakata shingo naaminika kuwa mtaalamu wa maswala ya kompyuta alisomea chuo kikuu cha Westminster.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC bwana huyo anaaminika kuwa alikwenda Syria mwaka wa 2012, lakini kabla ya wakati huo majasusi wa Uingereza na Marekani walikuwa hawajajua tishio lake.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment