June 04, 2016

Bondia maarufu wa Marekani ambaye ametamba sana enzi akiwa ulingoni, Muhammad Ali amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko nchini Marekani.
Muhammad Ali alifikishwa katika hospitali ya Phoenix Arizona baada ya kusumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji. Ali alifikishwa hospitalini siku ya Alhamisi na usiku wa kuamkia leo taarifa kutoka kwa msemaji wa familia zimeeleza kuwa amefariki dunia.

 
Madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu tayari walishawaasa wanafamilia kwamba hali ya bondia huyo ilikuwa mbaya sana na hakukuwa na dalili za yeye kuweza kupona. Jana ililazimika kuwekewa mashine yakumsaidia kupumua baada ya mfumo wake kushindwa kufanya kazi vzuri.
Bondia huyo alifikishwa hospitali January 2015 baada ya kupata tatizo katika mfumo wa mkojo lakini pia Disemba 2014 alifikishwa hospitali akisumbuliwa na pneumonia.
Mabondia wengine duniani kama Sugar Ray Leonard, Manny Pacquiao waliwataka watu kumwombea Muhammad Ali wakati alipokuwa hospitali akipatiwa matibabu.
Kwa miaka ya hivi karibuni, Muhammad Ali amekuwa haonekani hadharini pengine ni kutokana na hali yake ya afya haikuwa nzuri. Ali alizaliwa mwaka 1942 na amefariki mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 74. Ali alianza ubondia alipokuwa na miaka 12, na mwaka 1964 alishinda mashindano uzani wa juu duniani.
Muhammad Ali aliwahi kufikishwa mahakamani kwa kukaidi amri ya kujiunga na jeshi la Marekani wakati nchi hiyo ilipokuwa katika vita na Vietnam, lakini baadae mahakama ilimuachia.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE