February 23, 2015

 
Mtangazaji Maimartha Jesse na staa wa Bongo Fleva,Chege Chigunda wameingia kwenye bifu baada ya mtangazaji huyo kupost picha mtandaoni ikimuonyesha Chege akiwa jukwaani huku amefunga kitambaa cheusi mkononi na kuandika ….Angalia mkono Wa kushoto Wa chegge @chegechigunda hiiii ni hirizi ? any way isiwe kesi jiachie chege ila mziki mziki wako naupenda hata ukiniroga saw a Tu...japo cna imani hiyoo .
 
Akizungumza kwenye Uheard na Soudy Brown Chege alisema kuwa amemshangaa sana mtangazaji huyo baada ya kupost picha hiyo na kusema kuwa hiyo siyo hirizi bali ni kitambaa cheusi ambacho alikivaa alipokuwa kwenye shoo mkoani Dodoma lengo ni kumuenzi msanii mwenzake Mez B aliyefariki dunia wiki iliyopita mjini humo. ‘’Jamani hiyo siyo hirizi na huwezi kuvaa hirizi mchana kile kilikuwa ni kitambaa cheusi lengo lilikuwa ni kumuenzi Mez B,’alisema Chege.
Naye Maimartha Jesse akizungumzia suala hilo alisema kuwa hakuwa na nia mbaya ndiyo maana aliuliza ili watu wamwambie ni kitu gani amevaa Chege na mwisho alimuomba msamaha Chege baada ya kumkwaza kwa tukio hilo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE