Ras Six
Msanii wa muziki Ras Six, akiwa kama moja ya wanaharakati wa kutetea
haki za walemavu hususan watu wenye Albinisim, yeye mwenyewe akiwa mmoja
wao, amelaani mauaji yanayoendelea dhidi ya albino.
Amesema
kuwa kuna umuhimu wa vyombo vya habari na vyombo vya usalama
kuwahusisha zaidi katika vita vya kupambana na ukatili huo dhidi yao.
Ras Six amesema kuwa, kushirikishwa kwao zaidi katika vita hiyo
kutaongeza nguvu kutokana na wao kuguswa moja kwa moja na tatizo hilo na
kuweza kulielezea kwa undani zaidi, na vilevile msanii huyo akatumia
nafasi hii kulaani mauaji ya albino yaliyotokea hivi karibuni huko kanda
ya ziwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment