Akizungumza kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM leo moja kwa moja kutoka nchini Dubai alisema kuwa taarifa hiyo ameisikia na kwamba amekuwa akipigiwa sana simu na wadau mbalimbali kuhusiana na habari hizo na kusema kuwa ni jinsi gani watanzania wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya na habari hizo niza uzushi na hazina ukweli wowote. ‘’Taarifa hizo nimezisikia na nimepigiwa sana simu na watu mbalimbali kuhusiana na taarifa hizo lakini nimeona ni jinsi gani Watanzania wamekuwa wakitumia vibaya mitandao ya kijamii,ukweli ni kwamba Clouds FM na Tv havijauzwa kwa mfanyabiashara Rostam Aziz,’alisema Kusaga.
Aidha alisema kuwa hajaonana na mfanyabiashara huyo kwa miaka mingi na kuhusiana na taarifa kuwa Clouds FM inakibeba Chama Cha Mapinduzi(CCM) alisema kuwa Clouds Media kama chombo cha habari hakina chama wala dini na huwa inawapa nafasi viongozi wote wa vyama vya siasa.
‘’Kama ingekuwa ni kuwapendelea viongozi wa kisiasa basi ningempendelea Freeman Mbowe ni rafiki yangu zaidi ya miaka thelathini sasa,na naamini hii ni vita pengine maadui wetu wametengeneza ili kutuvunja moyo,naamini Mungu yu pamoja nasi na huwezi kufanya kitu bila yeye,’’alisema Kusaga.
Pia amezungumzia suala la ukatili na mauaji ya albino yanaendelea hapa nchini,suala la madawa ya kulevya nampongeza sana kamanda Nzowa na anafanya kazi nzuri ya kupambana na wauzaji wa madawa hayo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment