Kupitia mitandao ya kijamii wamepost picha na kulaani mauaji hayo.
diamondplatnumz Ndugu zangu! nafkiri ni Muda wa kubadilika sasa...Tuacheni fikra potofu, za Kipuuzi na ukatili Usio na Maana.. Hivi inamaa unataka kuniambia na hao kina Bill gates Mzee wa kuku, Carlos Slim, Amancio Ortega , Bakhresa na Matajiri wakubwa Duniani pia Walitajirika kupitia Ukatilii huu wa Ma Albino...??? Juhudi na Utendaji wako wa Kazi ndio utao kufanya Uendelee na kufikia Hayo Malengo unayoyataka... Tuache kujidanganya na Kuwatesa Ndugu zetu wasio na Hatia.....
ommydimpoz Kila mtu Anatamani kuwa na Mafanikio,Lakini Mafanikio hayaletwi kwa Kudhulumu nafsi ya Binadamu Mwenzio Kisa Utajiri,kwa pamoja tusimame na tupambane na Hawa watu wenye fikra potofu Wanaosaka utajiri kwa Kuua ndugu zetu Maalbino#StopAlbinoKillings
auntyezekiel STOP KILLINGS ALBINO HUYU PIA NI NDUGU RAFIKI NA MTU MUHIMU KTK JAMII YETU....
mdimuz Ni kweli mimi ni Albino, nimejikubali na nimeishi maisha yangu yote bila kujali nilivyo. Sijawahi kutumia hali yangu kupata kitu kwa huruma, nimeyapigania maisha yangu na nimepiga hatua.
Leo hii naongea nanyi nikiwa Baba, Mume, Mwandishi Mwandamizi, Blogger, na mengine mengi, lakini hali yangu sasa inaanza kunikwaza.
Haya mauaji jamani, nimejiteua kuwa Balozi, nitatetea, na kusimama mbele ya wenzangu wote wenye hali kama hii, kama ni wanasiasa ama wafanyabiashara, wanataka kutuua kwa maslahi binafsi, mwaka huu HAPANA.
Wanaoniunga mkono mikono juu

0 MAONI YAKO:
Post a Comment