February 23, 2015

 
 Kamanda wa polisi mkoa Morogoro

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Erick Bruno mkazi wa Manzese Tip Top Dar es salaam kwa kosa la mauaji.

Akitoa taarifa hiyo kwa mtandao huu ofisini kwake mapema leo hii, kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro RPC  Leonard Paul amesema,Mtuhumuwa ndugu Erick Bruno mwanye umri wa miaka 30, anatuhumiwa kwa kosa hilo la kumyonga mpaka kufa bi Jada Dungu anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 30-35 mkazi wa kichangani.
          
  tukio hilo limetokea Tarehe 23/02/2015 saa sita na nusu usiku (00:30) katika nyumba ya kulala wageni ya Stav iliyopo mtaa wa Kalakana kata ya kichangani inayomilikiwa na Paschal John Mafikiliambayo mtuhumiwa alikodi chumba namba 8

 Kwa mujibu wa taarifa za awali zinasema, siku ya tukio marehemu alisikika akipiga kelele akiomba msaada akiwa ndani ya chumba na mwanume huyo, ndipo mlinzi wa Gest hiyo alienda kuwagongea akiwataka wafungue mlango, lakini mwanaume huyo alijibu hakuna tatizo. Ndipo mlinzi aliita watu na kuvunja mlango wa chumba hicho na kukuta marehemu akiwa amenyongwa shingoni mpaka kufa 

 Hata hivyo chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na jeshi la polisi linaendelea na mahojiano na mtuhumiwa na upelelezi utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE