Kikosi cha TP Mazembe cha Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Timu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya
kidemokrasia ya Kongo imewasajili wachezaji watatu wapya toka kwenye
timu ya taifa ya Ivory Coast.
Nyota hao ni Roger Assale, Sylvain Gbohouo na Christian Kouame.
Wachezaji
hao wamejiunga na Mazembe wakitokea timu ya Sewe Sports kwa mkataba wa
miaka mitano ili kuweza kuisaidia timu kwenye ligi ya mabigwa Afrika.
Mshambuliaji Assale na golikipa Gbohouo walikuwemo kwenye timu ya Ivory Coast iliyotwaa ubigwa wa Afrika huko Guinea ya Ikweta.
Huku kiungo Kouame akishiriki kwenye timu ya taifa katika hatua za awali za kufuzu kwa michuano hiyo.
Rais
wa Tp Mazembe Moise Katumbi amewaelezea wachezaji hao "ni wachezaji
wazuri tunadhani wataleta mabadiliko makubwa, lengo letu ni kuwapa
nafasi wachezaji wa Kiafrika wenye vipaji."
Mabigwa hao wa Afrika
kwa mara nne watachuana na Mamelodi Sundowns mwezi ujao katika hatua za
awali za michuano ya ligi ya mabigwa Afrika
0 MAONI YAKO:
Post a Comment