Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) MKoani Arusha, Robson Meitinyiki,
amemtaka Katibu wa halmashauri Kuu (Nec) Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye, kuchunga kauli zake dhidi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward
Lowassa.
Hayo
ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
juu ya kauli ya Nape dhidi ya Lowassa kuwa, amepoteza sifa ya kuwa
mgombea wa uraisi kupitia chama hicho kwa kuyatuma makundi mbalimbali
kujifanya yanamshawishi kuchukua fomu.
Amesema anapaswa kuelewa chama hicho kilibomoka na ni chama cha watu
wote na kwa sasa chama kimeanza kuimarika kupitia jitihada za Katibu
Mkuu, Abdurahamani Kinana na yeye anaanza kujinyanyua na kutaka
kukibomoa.
Robson amesema Nape aelewe nyuma ya Lowassa wapo wengi na Arusha
wanajipanga kwenda kumshawishi achukue fomu na yeye hapaswi kutoa maneno
ya kejeli, kwani kuna kanuni na taratibu za vyama vya kumsimamisha mtu
kuwa mgombea, kama ana mgombea wake amtangaze japo lazima apitishwe na
chama,siyo mtu mmoja.
Aidha amesema kama Edward Lowassa anafanya maigizo, ili apendwe na
watu, basi wanamshauri mgombea wa Nape afanye maigizo hayo, ili apendwe
na watu kwa kufuatwa nyumbani kwake.
Amesema Nape aache watu wamfuate Lowassa na kumshawishi kwani sauti
ya watu wengi ni sauti ya Mungu na pia Mwenyekiti taifa alishasema watu
wamshawishi,na kauli zake zinaturudisha nyuma kutekeleza maagizo ya
Kinana aliyowaachia,kukijenga chama.
Naye Katibu Mwenezi Mkoa wa Arusha, Isack Joseph,Amesema Nape afike
mahali achunge kauli zake dhidi ya Lowassa, kwani Lowasa ni mtu mwenye
heshima katika nchi hii na alikuwa Waziri Mkuu na kuiletea taifa heshima
kubwa, hivyo vema vikao ya CC na NEC viachiwe viamue.
Amesema Kinana ameweka heshima kwa chama na kuondoa dhana ya
kutoleana heshima ya kupachikana majina ya magamba na sasa chama
kimerudi kwenye chati yeye Nape anataka kurudisha nyuma.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment