Mwenyekiti wa UDp, John Cheyo.
Dar es salaam. Mbunge wa Bariadi Mashariki na Mwenyekiti wa
Chama cha UDP, John Cheyo amesema wanakaribisha wanachama wa chama
chochote cha siasa nchini kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam, kiongozi
huyo alisema chama hicho bado hakijateua mgombea urais hivyo milango
iko wazi kwa wanasiasa ambao wako tayari kujiunga na chama hicho kwa
lengo la kuwania urais.
“Hiki chama ni cha watanzania wote hivyo tunatoa
rai kwa mtu yeyote aliye tayari kuwa mwanachama wetu milango ya kuwania
urais kupitia chama hiki ipo wazi’’ alisema Cheyo
Alisema yeye bado hajaamua kuwania nafasi hiyo
kwa sasa muda ukifika atasema lakini kwa sasa ni mapema kutoa tamko
kwamba atawania wadhifa huo.
Aliongeza kwamba anasikitishwa na Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa) kuwahamasisha watu wasipigie kura Katiba
inayopendekezwa, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwanyima haki wananchi.
‘’Raia wote wana haki ya kupiga kura sasa ikiwa
Ukawa wanatembea kila kona ya nchi kuwahamasisha wananchi kuacha
kuipigia kura katiba hiyo ni kosa,’’ alisema Cheyo
Pia Kiongozi huyo wa UDP alisema tume ya uchaguzi
ndio yenye majibu ya mashine zinazotumika kuandikisha wapiga kura
kwenye daftari la kudumu, (BVR) kwamba zinafaa au hazifai.
Alisema anashangazwa sana na baadhi ya watu
hususan wanasiasa na wasomi wanaojitokeza na kusema mchakato wa
kuandikisha wapiga kura usimamishwe kwa sababu zao mbalimbali .
Chanzo: Mwananchi.co.tz
Chanzo: Mwananchi.co.tz
0 MAONI YAKO:
Post a Comment