Akizungumza nje ya ukumbi wa bunge mara baada ya kikao cha Bunge kumalizika leo majira ya saa 5 Asubuhi, Makinda amesema kuwa anasubiri barua rasmi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo ndiyo itakayompa mwongozo kuhusu ubunge wa Zitto Kabwe.
Amesema kwa mujibu wa taratibu, kama chama kikimvua uanachama mbunge, kinapaswa kuiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo nayo inatoa mwongozo kwa bunge, jambo ambalo halijafanyika hadi sasa.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Mh. Tundu Lissu alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema kuwa anayetakiwa kuandika barua hiyo ni Katibu Mkuu wa Chama, na si yeye na kwamba hajapata taarifa kama barua hiyo imeandikwa au la..!
0 MAONI YAKO:
Post a Comment