March 31, 2015

Ummul-Khayr Sadir Abdul (19).

Vyombo vya usalama nchini Kenya, vinawashikilia wasichana watatu akiwamo Mtanzania, kwa kile kunachodaiwa kutaka kujiunga na kundi la kigaidi la al-Shabaab huko Somalia.

Taarifa kutoka kwa Kamishna wa Polisi Jimbo la El -Wak, mpakani mwa Kenya na Somalia, Nelson Marwa amesema Mtanzania aliyekamatwa, alijieleza kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika, Sudan.

Mtanzania huyo, Ummul-Khayr Sadir Abdul (19), mwenyeji wa Zanzibar, anatajwa kuwa kiongozi wa kundi hilo lililopanga kujiunga na al-Shabaab.

Wasichana wengine waliokamatwa pamoja na Ummul-Khayr, ni Maryam Said Aboud na Khadija Abubakar Abdulkadir wote raia wa Kenya.

“Hawa wasichana watatu, inaaminika kuwa walikuwa wanakwenda Somalia kupata mafunzo ya kigaidi na baadaye kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga,” alisema Kamishna Marwa.

Akizungumzia suala hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Diwani Athumani alisema: “Tunafuatilia hatujapokea taarifa zaidi ya hizo.”

Kamishna Marwa alisema raia hao wawili wa Kenya, mmoja ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya kilichopo Thika, Jimbo Kiambu na mwingine ni mwanafunzi wa Sekondari ya Burhania, iliyopo Malindi, Kilifi.

“Serikali imepata taarifa kuhusu watu wanaokusanya watu kutoka Afrika Mashariki ili wakajiunge na makundi ya ugaidi nchini Somalia, wakala wetu wa usalama wamepata taarifa hizo na kufanikisha kukamatwa kwa wasichana hao,” alisema Kamishana Marwa.

Hivi karibuni, tovuti ya al-Jazeera ilitoa taarifa za kukamatwa kwa mkanda wa video ulioonyesha mwakilishi wa kundi la kigaidi la Dola ya Kiislamu ya Iraq na Levant (ISIL) akimtaka kiongozi wa kundi la al-Shabaab kuliimarisha kwa kufanya mashambulizi ya kigaidi katika miji ya Mwanza na Dar es Salaam.

Kamishna Marwa alisema ingawa nyaraka za wasichana hao zote zinaonyesha kuwa ni wanafunzi, lakini bado walibanwa kwa maswali kuhusu sababu inayowapeleka nchini Somalia.

Aliongeza zaidi kuwa chanzo cha habari cha kiusalama kilieleza kuwa nyaraka za wasichana hao zilionyesha kuwa walikuwa wakienda kuolewa na wanajeshi wa kundi la al-Shabaab.

Related Posts:

  • Mtoto wa Waziri Mkuu auawa kwa kisu   Mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania marehemu, Edward Moringe Sokoine, Kereto Sokoine ameauwa kwa kuchomwa kisu katika ugomvi ulitokea na mkewe hii leo mkoani Arusha. Kamanda wa Polisi mkoa wa … Read More
  • Tundu Lissu aongea kwa mara ya kwanza, Sauti yake hii hapa Hali ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, imezidi kuimarika baada ya leo kutoa sauti yake akiongea na jamii kwa jumla na kuwaomba wazidi kumuombea. Lissu akiwa Hospitali nchini Kenya ametoa kauli hii . Bofya Video… Read More
  • Jibu la Lulu kuhusu kesi yake   Muigizaji Elizabeth Michael (Lulu), amesema kesi inayomkabili ya kuua bila ambayo inamkabili haikuwahi kuisha kama baadhi ya watu wanavyodhani. Muigizaji huyo  huyo anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo… Read More
  • Zitto atuma waraka mzito kwa Mh. Lissu Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama – ACT Wazalendo , Zitto Kabwe amesema kuwa amefarijika sana kusikia sauti ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa hospitali Nairobi baada ya sauti yake kusikika jan… Read More
  • Utafiti unaonesha Watanzania wanataka Katiba mpya   Utafiti wa Twaweza Tanzania unaonyesha kuwa asilimia 67 ya Watanzania wanasema ni muhimu kwa Tanzania kupata katiba mpya na asilimia 56 wanasema toleo la mwisho la rasimu ya katiba lipigiwe kura na wananchi. Ha… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE