Mwanasheria mkuu wa chama cha upinzani nchini CHADEMA, Tundu Lissu leo ametangaza kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kasikani Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam utupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.
"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa CHADEMA
Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.
Licha ya kutupilia mbali kesi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, Mahakama kuu imemtaka kulipa gharama zote za kesi toka ilivyoanza.
Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili na hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.Kwa maana hiyo basi kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi, mbunge yeyote au kiongozi wa kiserikali aliyechaguliwa na wananchi kupitia chama cha kisiasa, uongozi wake unakoma pindi anapovuliwa uanachama, kuama chama ama kufariki. Kwa maana hiyo Zitto Kabwe amevuliwa ubunge wake
Hata hivyo baada ya uamuzi huo Mwanasheria Alberto Msando ambaye ni Wakili wa Zitto Kabwe ameandika haya kwenye akaunti yake ya Instagram
Hii hapa sauti ya Zitto Kabwe akizungumza na Millardayo.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment