Mwanamuziki ambae amekuwa mstari wa mbele kutetea na kupiga vita dhidi
ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania Mwana FA ambae
kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Kiboko Yangu amefunguka na kuonyesha
hisia zake kali dhidi ya
watu
ambao tayari wamekutwa na hatia ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa
ngozi na kutaka watu hao wanyongwe haraka ili liwe funzo kwa watu
wengine wenye tabia hizo au kwa wale ambao wanafikiri kutaka kufanya
unyama huo dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi,Mwana Fa amefunguka hayo
leo kupitia kurasa wake wa Twitter na Facebook.
Mwana FA anadai kuwa kama nchi ikitekeleza adhabu hiyo kwa haraka na
kwa uwazi itasaidia kuifanya jamii iamini kuwa kweli nchi ipo makini na
ipo Serious na suala la mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa
ngozi.
"Inachukua muda gani hawa wanaopatwa na hatia ya kudhuru ndugu zetu
maalbino kunyongwa? Naona kama wangechinjwa mapema ingesaidia wapuuzi
wenzao kujua nchi ipo serious"
Wiki iliyopita watuhumiwa wannne wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa
ngozi walikutwa na hatia na kuhukumiwa kunyongwa ingawa bado mpaka sasa
hakuna mtu hata mmoja ambae amekwisha nyongwa,ndipo hali hii ilipoibua
maswali kwa msanii huyo kutaka kujua ni muda gani adhabu hii inaweza
kutekelezwa ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wanampango wa
kufanya ukatili na unyama dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment