Ushiriki wa uwekezaji mkubwa wa
kigeni kwa mwaka 2014 uliyawezesha masoko ya hisa ya kikanda kuweka
rekodi katika kupata mafanikio kwa wawekezaji wengi kupata marejesho
mazuri, hususan Soko la Hisa la Dar es Salaam, DSE nchini Tanzania,
lililotajwa kuwa soko bora la hisa kuliko yote barani Afrika kwa mwaka
uliopita.
Kipimo cha kampuni za ndani kilipanda kwa asilimia 27 mwaka jana, kiwango ambacho ni cha juu kabisa katika Afrika.
Mwezi
Agosti mwaka uliopita, Tanzania iliondoa kiwango cha mwisho cha
asilimia 60 kwa wawekezaji wa nje, na kufanya hisa za baadhi ya kampuni
kubwa kuliko zote na zenye kupata faida kubwa kupatikana kwa raia wasio
Watanzania kwa mara ya kwanza katika miaka mingi iliyopita. Uingiaji wa
fedha za kigeni kumeboresha ufanisi wa masoko ya hisa.
Kwa mujibu
wa makampuni zinazoripoti habari za kifedha duniani, Bloomberg, CBS na
Thomson-Reuters, Soko la Hisa la Misri lilishika nafasi ya pili kwa
kipimo chake kikuu kufikia ongezeko la asilimia 31.6 wakati Soko la Hisa
la Uganda, USE, lilibuka katika nafasi ya tatu kwa asilimia 26.5. Soko
la Hisa la Nairobi, NSE, lilishika nafasi ya nne, liliporomoka na
kuapata asilimia 19.2
Soko la Hisa la Tanzania, DSE pia lilikuwa
soko bora kuliko yote ya hisa barani Afrika kwa upande wa mtaji wa soko,
ambao ulikuwa kwa asilimia 40 kufikia dola za Kimarekani bilioni
$12.04, wakati hisa za ndani zikipanda kwa asilimia 66 kwa mwaka huo.
Mkuu
wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, DSE, Moremi Marwa amesema matokeo
hayo yameonyesha imani kubwa ya wawekezaji katika soko la DSE
kulikosababishwa na kuwepo mageuzi ambayo yana faida kwa uchumi wa
Tanzania.
"Tuliweza kuwavutia wawekezaji wa nje katika soko hili
walioshiriki katika soko lisilo na riba ya kudumu na upande wa mapato
kamili ya soko letu. Pia tulianzisha mtandao wa WAN, ambao umeruhusu
madalali kuingia katika miundombinu ya biashara na miamala na kuongeza
saa za biashara," amesema Bwana Marwa.
Mwaka uliopita, Tanzania
ilishuhudia kiwango chake kilichoorodheshwa cha soko kikipanda kwa soko
la hisa kuweza kusajili kampuni tatu za ndani na nyingine kutoka Kenya.
"Mwaka
2014, tulifanikiwa kuorodhesha kampuni ya Maduka Uchumi kutoka soko la
Hisa la Nairobi, Maendeleo Bank, Mkombozi Commercial Bank, na Swala
Energy. Tunatarajia kuorodhesha kampuni tatu zaidi kufikia mwishoni mwa
mwezi Aprili, ambao mbili kati yake zitakuwa katika Soko la Ukuaji wa
Kampuni na nyingine katika soko kuu," amesema Bwana Marwa.
"Tunaangalia matokeo ya muundo wa sasa ili tuone uzito wa mahitaji ya dhamana za serikali yetu kutoka ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki, EAC. Mara tukifanya hivyo, tutaweza kufungua ushiriki katika masoko yetu kwa sehemui nyingine ya dunia," amesema Bwana Maganga.
Awali, Tanzania iliruhusu wawekezaji kutoka ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki tu, kununua dhamana za serikali kufikia asilimia 40 ya dhamana za serikali zilizowekwa katika soko kununua zaidi ya theluthi mbili ya mgawo wa asilimia 40.
Kampuni ya saruji ya Tanzania, kampuni ya pili kwa ukubwa ya utengenezaji saruji, ilikuwa moja ya kampuni zilizofanya vizuri kabisa ikipata marejesho ya asilimia 124.2 mwaka kwa mwaka. Kampuni nyingine zilizokuwa katika kiwango cha juu ni Twiga, ambayo ilipata asilimia 50; Kampuni ya Bia ya Tanzania,TBL, ambayo ilipata asilimia 76; CRDB Bank ilipata asilimia 54 ambapo kampuni ya Sigara ilipata asilimia 94. Swiss port ilipata asilimia 87, DCB Commercial Bank alipata asilimia 47 wakati ambapo Benki ya National Microfinance ilipata asilimia 30.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment