Rais Uhuru Kenyatta Wa Kenya ametangaza siku 3 za maombolezo na
bendera kupepea nusu mlingoti kufuatia shambulio la kigaidi dhidi ya
Chuo Kikuu cha Garissa lililoua karibu watu 150. Akilihutubia
taifa kutoka Ikulu ya Nairobi, Rais Kenyatta amesema taifa hilo
halitaruhusu kundi la al-Shabaab la Somalia kuendeleza harakati zake za
kutaka kuwagawanya wananchi kwa misingi ya
dini. Amesema Uislamu ni dini ya amani na wananchi hawapaswi kuingia
kwenye mtego wa kundi hilo la kigaidi kwa kugawanywa kwa misingi ya
dini. Huku hayo yakijiri,s uala la mashambulizi ya Garissa limetawala
Kongamano la Kiislamu la kila mwaka katika jumba la Mikutano la KICC
jijini Nairobi. Viongozi Wa kisiasa nchini humo wakiongozwa na Waziri
wa Mashauri ya Kigeni Balozi Amina Muhammad, wamelaani ukatili huo
waliyoutaja kuwa kinyume na mafundisho ya Uislamu. Kadhalika viongozi
wa Baraza Kuu la Waislamu nchini humo Supkem, waliohudhuria kongamano
hilo, wameyataja mauaji ya Garissa kuwa ya kikatili huku wakitoa wito
kwa viongozi wengine wa kidini kutoa mafunzo sahihi ya Uislamu na
kuwatahadhari
SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA KUKABILI MAAFA SUMBAWANGA
-
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na UNDP, imezindua
nyaraka tatu muhimu za usimamizi wa maafa katika Wilaya ya Sumbawanga,
mkoa...
1 hour ago
0 MAONI YAKO:
Post a Comment