Al-Douri
Runinga nchini Iraq imeripoti kuwa
Izzat Ibrahim al-Douri, ambaye wakati mmoja alikuwa makamu wa Rais
Saddam Hussein na ambaye alitajwa kama nguzo kuu katika mchipuko wa
kundi la Islamic State nchini Iraq, ameuawa.
BBC bado haijapata
taarifa rasmi ya kuthibitisha kifo chake, lakini picha na maelezo kuhusu
kifo cha Bwana Al Douri imeripotiwa pakubwa.Iwapo taarifa hiyo ni kweli, kifo chake kitakuwa hatua kubwa kwa serikali ya Iraq dhidi ya makundi ya Jihadi.
Al Douri ambaye daima ana masharubu mekundu, alikuwa mfalme katika kilabu kwenye kadi zilizotolewa ili kusaidia majeshi ya Marekani kutawambua wanachama katika utawala wa Saddam Hussein, mnamo mwaka 2003.
Chanzo: BBC
0 MAONI YAKO:
Post a Comment