April 28, 2015

Watanzania wengine 20 kurejea kutoka A/Kusini 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza kuwa, Watanzania wengine 20 waliolazimika kuyakimbia makazi yao huko Johannesburg nchini Afrika Kusini wako salama na wiki hii wanatarajiwa kurejeshwa nyumbani baada ya kuibuka wimbi la hujuma na mashambulio dhidi ya wageni nchini humo. Kundi la kwanza la Watanzania 26 wanaoishi nchini Afrika Kusini lilirejea nyumbani Jumamosi iliyopita baada ya kushadidi hujuma na mashambulio dhidi ya wageni. Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga amesema kwamba, serikali inakamilisha utataribu wa kuwatambua Watanzania wengine 20 waliobakia ambao watarejeshwa nyumbani. Amesema kuna haja ya kuhakikisha uraia wao kuna kuna wengi ambao wanadai kuwa ni Watanzania na wanazungumza vizuri Kiswahili lakini kiuhakika sio raia wa Tanzania. Wakati huo huo, habari kutoka nchini Afrika Kusini zinasema kuwa, hali ya mambo nchini humo imeanza kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya majuma kadhaa ya hujuma na mashambulio dhidi ya raia wa kigeni.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE