May 17, 2015

Aunty Ezekiel afunguka sababu ya kutomualika Wema kwenye sherehe yake 
 Uhusiano wa mastaa wawili wa Bongo Movie,Wema Sepetu na Aunty Ezekiel wadaiwa kuwa tete sababu kubwa ikielezwa kuwa Aunty kupost kwenye akaunti yake ya Instagram tangazo la shoo ya Zari White Party iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu Mlimani City,jijini Dar.
Sababu nyingine inayofanya mashabiki kuamini mastaa hao kuwa wamegombana ni hivi karibuni Aunty Ezekiel kufanya sherehe ya Baby Shower iliyofanyika kwenye  Bustani za Ndoto Polepole zilizopo Bagamoyo,Pwani kumualika hasimu wa Wema,Kajala,ambapo Wema hakuwepo.
wema 
Katika sherehe hiyo Wema hakuwepo,hata hivyo Aunty Ezekiel aliizungumza na Uheard ya Soudy Brown,alisema kuwa hana ugomvi na Wema na sababu ya kutomualika kwenye sherehe yake ni kuwa msanii huyo alikuwa anashuti filamu.
‘Sijagombana na Wema,sikumualika kwenye baby shower kwa sababu alikuwa bize anashuti video,’alisema Aunty.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE