May 17, 2015

Nouri Al-Maliki: Kuna nchi zinataka kuigawa Iraq 
Makamu wa Rais nchini Iraq amesema kuwa baadhi ya nchi katika eneo la Mashariki ya Kati zinaendesha sera zenye lengo la kuivuruga na kuigawa nchi yake. Nouri al-Maliki amesema, mipango yoyote ya kuigawa Iraq itakabiliwa na upinzani wa kila kona kutoka kwa wananchi ambao siku zote wamesimama kidete kutetea umoja wa taifa lao. Hii ni katika hali ambayo, baadhi ya nchi za Kiarabu zinashirikiana na Marekani kuigawa Iraq katika majimbo matatu. Muswada uliowasilishwa kwenye Congress ya Marekani unataka Iraq igawanywe mara tatu na wapiganaji wa Kikurdi waweze kupewa silaha moja kwa moja kutoka Washington bila ridhaa ya Baghdad. Kiongozi wa Kishia nchini Iraq, Muqtada al-Sadr ameionya Congress dhidi ya kupitisha muswada huo. Nouri al-Maliki, makamu wa rais wa Iraq amesema muswada huo una mkono wa baadhi ya nchi za Kiarabu za Mashariki ya Kati.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE