Burundi:Nkurunziza ahairisha uchaguzi
Rais wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi .
Msemaji
wa rais Willy Nyamitwe ameiambia shirika la habari la AFP kuwa kufuatia
jaribio la mapinduzi juma lililopita na vurugu zilizofuatia ni bora
kuahirisha uchaguzi huo kwa muda.''Uchaguzi huo wa ubunge ulikuwa umeratibiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Mei lakini sasa inatubidi kuihairisha ili kuwasikiza washirika wetu wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi ambayo pia inatumia muda huo kutatua maswali yaliyoulizwa na vyama vya upinzani.'' alisema Nyamitwe.
Hadi kufikia sasa tarehe rasmi ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanywa Juni tarehe 26 haijabadilika.
''Subiri tu'' Nyamitwe aliwaambia waandishi wa haba
Wanajeshi waaminifu kwa Nkurunziza walizima jaribio la mapinduzi juma lililopita
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba amesema kuwa tayari rais
Nkurunziza ametia sahihi amri hiyo ya kuhairishwa kwa uchaguzi.
Umoja
wa mataifa ya bara Ulaya EU, na Umoja wa mataifa ya Afrika AU, yametoa
wito kwa uchaguzi huo uliokumbwa na utata mkubwa uhairishwe ilikutoa
fursa kwa mazungumzo ya upatanishi kuendelea .
Hapo jana Rais wa
Afrika Kusini alitilia pondo hoja hiyo ya kuahirisha uchaguzi akisema ni
bora uchaguzi huo uliopangwa ''uhairishwe''.
Takriban watu 20
wameuawa kufuatia makabiliano baina ya polisi na waandamani katika mji
mkuu wa Bujumbura kilele ikiwa ni juma lililopita makamanda waasi
walipotangaza jaribio la mapinduzi rais
Nkurunziza akiwa mjini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kanda uliolenga kutatua mzozo wa kisiasa nchini mwake.
Waandamanaji wamekuwa wakipinga kauli ya Nkurunziza ya kutaka kuwania muhula wa tatu
Wapinzani wa rais Nkurunziza wanasema kuwa kutangazwa kwake nia ya
kuwania muhula wa tatu unakiuka sheria na makubaliano ya amani ya mwaka
wa 2006 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka
13.Nkurunzizakwa upande wake anashikilia kukutu kuwa ana haki ya kuwania muhula mwengine kwani muhula wa kwanza hakuchaguliwa na wanainchi bali wabunge.
Takriban watu laki moja wamekimbilia mataifa jirani wakihofia kutibuka upya kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment