Viongozi wa dini, wanasiasa na wazee nchini wamewaonya
Watanzania kujiepusha na viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Viongozi hao walisema hayo, Dar es Salaam jana katika Mkutano kuhusu
Amani na Utulivu wa Tanzania, ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu
Nyerere. Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi
hiyo, Dk Salim Ahmed Salim, alisema ni wakati sasa wa Watanzania kuanza
kuchukua hatua za kulinda amani iliyodumu kwa muda mrefu na kuipatia
sifa ndani na nje ya nchi. Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba
alisema tayari taifa la Tanzania limeanza kuwa na viashiria hatari vya
uvunjifu wa amani, hali inayolazimu kuchukuliwa hatua za haraka ili
kuhamasisha umoja na mshikamano. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, alitaja viashiria vilivyoanza kuonekana
nchini vya uvunjifu wa amani kuwa ni mauaji ya watu wenye ulemavu wa
ngozi (albino), wazee na vikongwe, migogoro ya kisiasa, ardhi, wakulima
na wawekezaji, kutoaminiana na kutotendewa haki sawa. Mwenyekiti wa
Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema msingi wa
amani siku zote ni kuwepo kwa haki, endapo haki itakosekana lazima
kutakuwepo na tatizo la amani.
May 20, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment