Mkurugenzi wa kundi la Mkubwa na Wanawe,Said Fella ‘Mkubwa Fella’ amempa
zawadi ya gari msanii wake kutoka kundi la Yamoto Band,Aslay katika
sherehe ya kuadhimisha miaka 20 ya kuzaliwa kwake.
Kupitia yake ya Instagram Aslay aliandika hivi kumshukuru Mkubwa Fella..
Asante mungu Kwa kunipa uhai Na kipaji ambacho leo hii kina fanya
naitwa Aslay pia nakushukuru kwa kunifikisha kwenye mikono Ya mtu mwenye
moyo wa kibinaadamu.
Najua kuna mengi makubwa ambayo boss wangu Mkubwa Fella umenifanyia
ambayo si vyema kuyataja yote kwasababu wakati wake haujafikia ila
naomba nichukue fursa hii kukushukuru kwa hiki ulichonifanyia leo katika
sherehe ya kusherehekea siku yangu Ya kuzaliwa umenifanya nijione
mwenye thamani kubwa duniani sikutegemea kama leo itakuwa siku yangu ya
kumbukumbu ambayo sitoweza kuisahau hata nije kuwa bilionea Mkubwa Fella
asante kwa kunipa hii zawadi ambayo mimi kama mimi sikuiwazia kabisa
kama leo nitapata gari.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment