
Kwa mara ya kwanza mwanamuziki wa Hip Hop toka mkoani Morogoro STAMINA kesho ataandika historia ndani ya mkoa huo kufuatia uzinduzi wa Albam yake ya MT. Uluguru
Uzinduzi huo utakaofanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri Morogoro utahudhuliwa na wakali kibao wa Bongo Fleva watakaotoka ndani na nje ya mkoa wa Morogoro. Wanamuziki kama Feed Q, Izoo B, Roma, Afande Sele, Madee, Barnaba, Rachel, Rich Mavoco, Darasa, MR. Blue, Mash J, Kenny, Poison na wengine kibao watamsindikiza Stamina katika uzinduzi huo.
Kiingilio kitakuwa ni TSH:5000/= na milango itakuwa wazi kuanzia saa nne kamili Asubuhi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment