June 20, 2015

 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kimesema hakuna sababu wananchi kubebeshwa mizigo ya michango isiyoisha wakati wanakabiliwa na changamoto za kukosa huduma za afya na maji.
Wakizungumza na wananachi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa kanisani kata ya ruaha wilayani kilosa viongozi wa chadema wa kata, vijiji na mitaa wamesema serikali inatumia fedha nyingi kukimbiza mwenge nchi nzima huku ikiwaacha wananchi wakiteseka na umaskini wa kutupwa.
Pia wamewataka wananchi kutoshughulishwa na watiania wa ccm bali wajiaandikishe ili kuwachagua viongozi watakaowaletea mabadiliko.
Naye katibu wa CHADEMA kata ya Ruaha Haji Mponda amesema CHADEMA haitawavumilia viongozi wa serikali za mitaa walio omba ridhaa kuongoza wananchi kupitia CHADEMA kwa lengo la kujinufaisha na kufanya ubadhilifu wa fedha za wananchi chama kitamshughulikia bila kujali muda aliomaliza kwenye madaraka.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE