June 05, 2015

 

Srikali ya Tanzania imeanzisha kituo cha kwanza cha tembo yatima mjini Arusha.
Kituo hicho kinatarajiwa kuhifadhi watoto wa tembo waliopoteza wazazi wao kutokana na vitendo vya ujangili au sababu nyengine.
Hatua ya serikali ya kuanzisha kituo hicho inakuja baada ya utafiti wa serikali kubaini kuwa Tanzania hupoteza takriban tembo 30 kila siku.
Kituo hicho kinatarajiwa kutoa uangalizi kwa tembo wadogo wapatao 40, na watahifadhiwa mpaka watakapokuwa wakubwa na hatimae kurudishwa katika mazingira yao halisia.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na BBC, waziri wa Utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu amebaini kwamba katika hifadhi ya taifa ya Ruaha pekee, tembo wapatao 12,000 walitoweka katika kipindi cha mwaka mmoja.
Waziri Nyalandu amekiri kwamba kiwango hicho ni kikubwa mno na kwamba kinatia wasiwasi hivyo kuongeza kwamba uchunguzi umefanyika kubaini chanzo cha tatizo hilo.
  
Mamlaka maalumu ya Umoja wa Mataifa inayojihusisha na wanyama walio hatarini, imesema kwamba takwimu hizo zinaashiria kwamba Tanzania ni kitovu cha ujangili huku pembe za ndovu zikisafirishwa kupitia bandari ya Dar es
Salaam kwenda nchi jirani.
Tangu mwaka 2009, angalau tani 45 za pembe za ndovu zinaaminika kusafirishwa kwa njia za magendo kutoka Tanzania.
Ripoti zinasema Kenya hupoteza mabilioni ya dola kila mwaka kutokana na ufisadi.

Related Posts:

  • Hatari ya huyu dogo ulipata kuona??    Hii kwa nchi zetu za Afrika hasa Tanzania ni hatari sana kwa mtoto kama huyu kucheza na nyoka. Lakini kw awenzetu ni kawaida sana. Ebu tazama Video hapa chini ujionee       &nbs… Read More
  • Makamu wa rais Burundi atoroka     Makamu wa rais Burundi anaaminika kuwa ametorokea Ubeljiji Moja kati ya makamu wa rais wa Burundi ametoroka nchini humo baada ya kutangaza kuwa anapinga hatua ya rais wa nchi hiyo Pie… Read More
  • Millard Ayo awatosa Lulu, Jokate   Mtangazaji mwenye sauti nzito Bongo kupitia Clouds FM, Millard Ayo. MTANGAZAJI mwenye sauti nzito Bongo kutoka Clouds FM, Millard Ayo, Jumatatu iliyopita alibanwa azungumzie uhusiano wake na warembo wenye majin… Read More
  • Waziri Membe akutana na wasanii wa filamu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wasanii wa tasnia ya filamu mkoa wa Morogoro jana, wakati alipokuwa mkoani hapa ku… Read More
  • Vanessa Mdee: KTMA 2015 imenipa nguvu ya kujituma zaidi Vanessa Mdee amesema ushindi wa tuzo mbili za Kilimanjaro Music Awards ikiwemo ya muimbaji bora wa kike, umemfanya apate moyo wa kujituma zaidi. Amedai kuwa ushindi huo pia ni ishara kuwa kazi anayoifanya i… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE