Diwani
wa kata ya Gongo la Mboto,Jerry Slaa ameainisha mafanikio aliyotekeleza
katika kipindi cha miaka mitano tangu achaguliwe kuwa Diwani na Meya wa
Manispaa ya Ilala ambapo pia alitimiza ahadi mbalimbali alizokuwa
ametoa kwa wakazi wa kata za manispaa ya Ilala.
Slaa
alivipatia msaada wa fedha vikundi vya VICOBA alivyokuwa ameviahidi
kuvisaidia, jeenereta za kutoa nishati za kuendeshea miradi kwa vikundi
kwenye maeneo yasio na umeme, vifaa vya michezo kwa vijana na hati za
uthibitisho wa ujenzi wa barabara zitakazojengwa kwa madiwani wa kata
za jimbo la Ukonga.
Slaa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu
ya Chama Cha Mapinduzi alitangaza mafanikio hayo katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi ya Kitunda iliyopo jimbo la
Ukonga jana ambapo pia alitangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la
Ukonga kupitia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika
Oktoba mwaka huu.
Baadhi
ya mafanikio aliyofanikisha katika kipindi cha uongozi wake
aliyabainisha kuwa ni katika sekta ya elimu- ambapo mazingira katika
shule mbalimbali yameboreshwa, afya-ambapo vituo vipya vimejengwa na
vingine kupatiwa vifaa na dawa,miradi ya maji na ujezi wa barabara
kwenye kata ya Gongo la Mboto na kata zote za Manispaa ya Ilala.
“Kutokana
na mafanikio yaliyopatikana nawaomba wananchi wa jimbo la Ukonga
mniunge mkono kwa kinichagua niwe Mbunge wenu katika uchaguzi mkuu ujao
ili nizidi kuwatumikia na kushirikiana nanyi kuleta maendeleo katika
jimbo hili la Ukonga ambalo bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali
za maendeleo ”Alisema.
Mkutano huo wa Meya, Jerry Slaa ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wengi wa jimbo la Ukonga ambao wengi wao walipokea tamko hilo la kutangaza nia kwa furaha na baadhi ya waliohojiwa walisema kuwa kiongozi huyo anaelewa matatizo ya wananchi wa Ukonga na ni mtu wa watu ambaye amekuwa akitekeleza majukumu yake ya kazi kwa kujali watu wa aina zote.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment