Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza daktari John Magufuli kuwa mgombea wake
wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa ujao.
Daktari John Magufuli, alisajili asilimia 87 % ya kura za wajumbe, hiyo ikiwa ni kura 2104.Daktari John Magufuli, aliwashinda wapinzani wake Bi Amina Salulm Ali na dakta Asha-Rose Migir.
Je Daktari John Magufuli ni Nani?
Mgombea wa urais wa chama cha
CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph
Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania.
Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera.
Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.
Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.
Aidha
daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema
miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT .
Alianza siasa mwaka 1995
Alipohitimu, daktari Magufuli
na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union
akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge.
Magufuli
alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda
kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa
Miundombinu.
Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.
Alianza siasa mwaka 1995
Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.
Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya
makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi.
Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti
Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.
Daktari
Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti,
mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.
Anatambulika kuwa Mchapa kazi
Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti.
Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.
Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.
Na alipokuwa waziri wa
Maendeleo ya Mifugo, Bwana John Magufuli alikwenda hadi bandari ya
Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina iliyokuwa inashukiwa kufanya
uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya Tanzania.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment