Akiongea kwenye mahojiano na jarida la Essence la Marekani, Vanessa amesema muziki ni kitu alichoamua kukipa muda wake wote kwa sasa tofauti na mwanzo ambapo alikuwa akifanya kazi ya utangazaji pia.
“Kwa sasa mimi ni msanii, mtumbuizaji, mchezaji muziki na staa wa rock wa 24/7, siku saba za wiki,” alisema kwenye mahojiano hayo na jarida hilo maarufu la nchini Marekani.
Kwenye mahojiano hayo waliyomfanyia visiwani Zanzibar, Essence wamemuelezea Vanessa kama msanii wa kike maarufu zaidi nchini Tanzania akiwa na followers zaidi nusu milioni kwenye mtandao wa Instagram na huku akifuatwa na mastaa kama Trey Songz na Kelly Rowland.
Vanessa Mdee aliyeshinda tuzo mbili za Kilimanjaro mwaka huu, anawania kipengele cha msanii bora wa kike kwenye tuzo za MTV MAMA zitakazofanyika Jumamosi ijayo jijini Durban, SA.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment