Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa pili
kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza majimbo
mapya ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
leo. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)
TUME ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majimbo 26 mapya ya uchaguzi ambayo
yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka
huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kukata kwa majimbo hayo
wamezingatia idadi ya watu pamoja na Jiografia katika majimbo mapya.
Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.
Majimbo
yaliongezwa ni Handeni Mjini, Nanyamba, Makambako, Butiama, Tarime
Mjini, Tunduma, Msimbo, Kavu, Geita Mjini, Mafinga Mjini, Ushetu, Nzega
Mjini, Kahama Mjini, Kondoa Mjini, Newala Mjini, Bunda Mjini, Mbulu
Mjini, Ndanda, Madaba, Mbinga Mjini, Mbagala,
Kibamba,Vwawa,Monongo,Mlimba, Pamoja na Uliambulu.
Jaji
Lubuva amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakiingia katika Halmashauri
mbili hiyo kuweka mipaka katika maeneo ili mbunge aweze kushiriki katika
Halmashauri moja tu.
Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa majimbo hayo kisheria.CREDIT: MICHUZI BLOG
0 MAONI YAKO:
Post a Comment