Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinasema zaidi ya abiria 20 wamefariki dunia usiku wa jana, huku zaidi ya abiria 40 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda Dar es salaam kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na kisha kupinduka.
Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma, hadi hivi sasa bado kuna miili haijatolewa kwenye mabaki ya basi hilo kutokana na kuharibika vibaya na kubaki mithili ya nyama.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment