
Wasanii
Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Saleh Kiba ‘Aki Kiba’ kesho Jumapili
wanatarajiwa kutumbuiza katika uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Diamond
na Ali Kiba ni sehemu ya wasanii wengi wa muziki na wale wa filamu
watakaotoa burudani kwenye uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika Viwanja
vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kitendo
cha Ali Kiba na Diamond kupanda jukwaa moja ni nadra kutokea kutokana
na upinzani uliopo kati yao, hiyo watu watakaofika kwenye uzinduzi huo
watapata burudani ya bure ya aina yake.

Mbali
na kutamba na nyimbo nzuri kwa kila mmoja wao, kumekuwa na upinzani
mkali kuhusu msanii mkali wa kutawala jukwaa, hivyo wawili hao
wanatarajiwa kutoa burudani ya kiwango cha juu ili kuendelea
kuthibitisha ubora wao.

Magufuli
amepata nafasi hiyo baada ya kupita katika mchujo wa watangaza nia
zaidi ya 40 waliojitokeza ndani ya CCM. Uchaguzi Mkuu unatarajiwa
kufanyika Oktoba 25, mwaka huu
Chanzo:seetheafrica.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment