Akizungumza jijini Dar es salaam afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF Baraka Kizuguto amesema hapo awali kocha wa timu hiyo Boniface Mkwasa aliita kikosi cha wachezaji 38 ambapo wachezaji watano wa kimataifa ambao ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngassa, Hassan Sembi na Ally Yusuph hawatakuwa na kikosi hicho kutokana na masuala mbalimbali.
Wachezaji walioitwa na kocha ambao wanatarajia kuingia kambini Jumapili asubuhi ni Walinda Mlango Ally Mustapha'Bartez' (Yanga), Aishi Manula(Azam Fc), Said Mohamed (Mtibwa Sugar).
Walinzi ni Shomary kapombe (Azam FC), Juma Abdul (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub Canavaro (Yanga), Haji Mgwali (Yanga), Mohamed Hussein Tshabalala (Simba), Abdi Banda (Simba) na Hassan Issihaka (Simba).
viungo wakiwa ni mudathir Yahya (Azam FC), Himid Mao (Azam FC), Frank Domayo (Azam FC), Simon Msuva (Azam FC), Salum Telela (Yanga), Deus Kaseke (Yanga), Said Ndemla (Simba).
Washambuliaji John Bocco, Rashid Mandawa (Azam), Farid Mussa (Azam FC).
0 MAONI YAKO:
Post a Comment