August 21, 2015



Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa mchezaji wake Jack Wilshere, atakosa michezo ya England kufuzu Euro 2016 dhidi ya San Marino na Switzerland itakayofanyika mapema mwezi ujao.
Wilshere miaka 23 anaendelea kupata nafuu baada ya kupata majeraha, bosi huyo wa Arsenal ambaye timu yake itakutana na Liverpool, Jumatatu usiku katika Premier League amesema" ni vigumu kudhani mchezaji huyo atakuwemo katika kikosi cha England hivi karibuni, nadhani baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa anaweza kuwa tayari kucheza lakini kwa sasa bado hayupo vizuri kucheza"anasema Wenger.


Kocha Wenger pia amewahakikishia mashabiki wa Gunners kuwa yupo sokoni kutafuta mchezaji mpya kabla ya kufungwa dirisha la usajili September mosi.
Aidha Mfaransa huyo amesisitiza kuwa mchezaji wake Mesut Ozil ambaye alitoa pasi ya goli kwa mshambuliaji wake Olivier Giroud katika mchezo dhidi ya Crystal Palace juma lililopita, kuwa yupo tayari kuonesha kiwango bora msimu huu.
Wenger miaka 65, amesema "Ozil ni mchezaji mzuri ambaye amekamilika kila kitu na mwenye kuweza kuleta matokeo chanya kwa timu yetu".

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE