Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilali
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilali ameihakikishia dunia kuwa
serikali ya Tanzania ina dhamira ya dhati ya kumaliza tatizo la
usafirishwaji haramu wa binadamu.
Dkt.
Bilal ameyasema hayo leo mbele ya Mabalozi na wawakilishi wa mashirika
mbalimbali yanayopinga usafirishwaji haramu wa binadamu waliohudhuria
uzinduzi wa sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu na Mpango
kazi wa kitaifa wa mwaka 2015-17 wa kumaliza tatizo hilo.
Dkt. Bilal ameongeza kuwa kuwa tatizo hilo ni kubwa duniani kote
ambapo takwimu zinaonesha kuwa watu laki saba husafirishwa kiharamu toka
nchi moja kwenda nchi nyingine kwa ajili ya kutumikishwa kazi za
mashambani, majumbani na hata kazi za ngono na ugaidi haswa vijana,
watoto na wasichana.
Kwa upande wake waziri wa mambo ya ndani Mathiasi Chikawe amesema
kuwa tafiti zinaonesha kuwa Tanzania inatumika katika upitishaji wa
wahamiaji haramu kwenda nchi nyingine za Afrika, Ulaya na Mashariki ya
mbali
0 MAONI YAKO:
Post a Comment